Raisi Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Prof.Benno T.Ndulu (pichani) kuwa Gavana wa Benki Kuu Tanzania (BOT). Uamuzi huo umefuatana pia na maamuzi mengine mazito kama ambavyo yameanishwa katika taarifa rasmi ya Ikulu iliyotolewa hivi leo jijini Dar-es-salaam. Yote haya yanafuatia utata na sakata zima lililokuwa limeigubika Benki Kuu ya Tanzania.
Wakati huo huo Raisi Kikwete amemteua Dr. Enos S.Bukuku kuwa Naibu Gavana wa Benki Kuu. Taarifa rasmi ya Ikulu unaweza kuisoma hapa.
TAMKO LA SERIKALI KUHUSU TAARIFA YA UKAGUZI WA HESABU KATIKA AKAUNTI YA MALIPO YA MADENI YA NJE (EXTERNAL PAYMENT ARREARS ACCOUNT – EPA) ILIYOKO BENKI KUU YA TANZANIA.Nafurahi kuwaarifu kuwa, kazi ya Ukaguzi wa Hesabu za mwaka wa fedha 2005/06 za Akaunti ya Madeni ya Malipo ya Nje yaani External Payment Arrears (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania imekamilika. Kazi hiyo ilifanywa na Wakaguzi wa Kampuni ya Ernst and Young kwa niaba ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali. Ilianza Septemba, 2007 na kukamilika Desemba, 2007. Juzi tarehe 07 Januari, 2008 Rais Jakaya Mrisho Kikwete alikabidhiwa Taarifa hiyo na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali. Rais ameisoma, ameifanyia kazi na kuitolea maamuzi.
Historia ya EPA
Katika miaka ya 1970 mpaka 1990 nchi yetu ilikuwa inakabiliwa na tatizo kubwa la upungufu wa fedha za kigeni. Benki Kuu ya Tanzania ilipewa jukumu la kusimamia matumizi ya fedha za kigeni kwa niaba ya Serikali. Benki Kuu ndiyo iliyokuwa na mamlaka ya kupanga na kuamua nani agawiwe fedha za kigeni na kiasi gani!
Kwa ajili ya kuwahudumia wafanyabiashara, mashirika na makampuni yanayoagiza bidhaa na huduma kutoka nje, Akaunti maalum ilifunguliwa katika Benki ya Taifa ya Biashara kwa wakati huo. Akaunti hiyo ilijulikana kwa jina la External Payment Arrears (EPA) au Akaunti ya malipo ya Madeni ya Nje, kwa tafsiri ya Kiswahili.
Waagizaji wa bidhaa au huduma kutoka nje waliwajibika kulipa kwenye Akaunti hiyo, fedha ya Tanzania yenye thamani inayolingana na fedha za kigeni zinazotakiwa kulipia bidhaa au huduma hiyo huko nje. Baada ya waagizaji wa ndani kufanya hivyo, kutegemeana na upatikanaji wa fedha za kigeni, wauzaji au watoaji huduma wa nje walilipwa. Benki Kuu iliamua nani alipwe na Benki ya Biashara ilifanya malipo.
Juni, 1985 iliamuliwa kuwa shughuli za akaunti hiyo zihamishiwe Benki Kuu kutoka Benki ya Taifa ya Biashara na zimeendelea kuwepo hapo mpaka sasa. Katika Benki Kuu kikaundwa kitengo maalum cha kusimamia na kuendesha shughuli za akaunti hiyo kilichojulikana kama Debt Management Unit chini ya Kurugenzi ya Sera (Directorate of Economic Policy).
Kwa sababu ya tatizo la upungufu wa fedha za kigeni kuendelea, malimbikizo ya madeni hayo yalizidi kukua mwaka hadi mwaka. Kwa mfano, mwaka 1999 deni hilo lilifikia dola za Kimarekani 623 milioni. Kati ya fedha hizo, dola 325 milioni ndilo deni la msingi na dola 298 milioni ni riba yake. Baadae likaongezeka kufikia dola 677 milioni.
Juhudi za Kulipa MadeniJuhudi za kulipa malimbikizo ya madeni hayo ziliendelea kadri fedha za kigeni zilipopatikana. Kwa nia ya kutaka kutafutia ufumbuzi wa haraka tatizo hilo na kupunguza mzigo wa madeni, Serikali ilianza kutafuta njia nyingine mbalimbali. Mwaka 1994, Serikali kwa kushirikiana na Benki ya Dunia ilianzisha Mpango wa Kununua Madeni (Debt Buy Back Scheme). Yaani waliokuwa wanaidai BoT waliombwa wakubali kulipwa sehemu tu ya madeni wanayodai. Wapo wadai kadhaa walikubali na madeni yao yakauzwa chini ya mpango huo. Taarifa za mwaka 2004 zinaonyesha kuwa madeni ya thamani ya dola 228 milioni yalilipwa chini ya mpango huu.Pili, Serikali ilifanya juhudi ya kupata msamaha wa madeni hayo kutoka nchi wanachama wa Paris Club. Serikali iliomba kuwa pamoja na kutusamehe madeni ya kiserikali toka nchi zao wasaidie tusamehe na madeni ya makampuni yao kwetu. Yapo pia madeni ambayo yamelipwa na makampuni ya Bima baada ya makampuni yaliyouza bidhaa na huduma Tanzania kushindwa kulipwa. Madeni ya dola 216 milioni yalihusika chini ya michakato hii. Hivyo basi, deni la dola 444 milioni lilipungua katika ile jumla ya dola 677 milioni. Kwa hiyo mwaka 2004 deni katika Akaunti ya Malipo ya Nje lilikuwa dola 233 milioni. Yalikuwepo mawazo ya baadhi ya watu kuwa pengine deni hilo lisilipwe au tulikatae. Walikuwepo waliokubali madeni yao yafutwe na wengine waliagiza fedha zao zipewe NGO. Lakini, baadhi ya wadai waliendelea kudai na wengine hata kushitaki mahakamani. Hivyo BoT ililazimika kuendelea kulipa kadri wadai walipojitokeza.
Ulipaji kwa IdhiniKatika utaratibu wa malipo ya madeni ya EPA kanuni zinaruhusu mdai kuamua deni lake kulipwa kwa mtu au kampuni nyingine. Kanuni zinamtaka mdai kutoa hati iliyothibitika kisheria ya yeye kuidhinisha malipo hayo yafanywe (Notarised Deeds of Assignments) hivyo. Pia yapo masharti ya kutimizwa na kampuni au mtu aliyeidhinishwa kulipwa hilo deni. Utaratibu umetumika kufanya malipo kadhaa ya madeni katika Akaunti ya EPA.
Matatizo ya Mwaka 2005/6Katika ukaguzi wa Hesabu za BoT za mwaka wa fedha 2005/6, Agosti, 2005 kuligundulika matatizo katika ulipaji wa madeni kwa utaratibu wa idhini ya kulipwa wakala wa mdai katika akaunti ya EPA. Kukajitokeza kutokuelewana kati ya Benki Kuu na Mkaguzi Deloitte and Touche’ aliyegundua tatizo hilo. Baadaye mkaguzi huyo alisitishwa kuendelea na kazi. Serikali ikaingilia kati na tarehe o4 Desemba, 2006 ilimuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuhakikisha kuwa ukaguzi wa akaunti hiyo unafanyika kwa kina. Aidha, ilimuagiza atafute kampuni ya kimataifa ya ukaguzi ifanye kazi hiyo kwa niaba yake. Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabau za Serikali, ndiye kwa mujibu wa Sheria ya BoT mkaguzi wa Hesabu za Benki Kuu. Hata hivyo kwa mazingira hayo maalum Serikali ilimtaka CAG atafute mkaguzi mwingine wa nje.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) alifanya hivyo na matokeo ya mchakato wa kutafuta kampuni hiyo uliochukua miezi mitano (Januari hadi Mei, 2007) ndipo ikapatikana kampuni ya Ernst and Young.UKAGUZI
Wakaguzi wa Kampuni ya Ernst and Young wakaanza kazi hiyo Septemba, 2007 na kuikamilisha Desemba, 2007. Wakaguzi hao wamefanya kazi nzuri iliyothibitisha kiwango cha juu cha weledi (Professionalism) cha wakaguzi hao. Tunawapongeza, tunawashukuru. Tunatambua kuwa walipata matatizo mengi hasa ya kupata taarifa zilizo sahihi kwa sababu ya matatizo ya utunzaji wa kumbukumbu. Madeni haya ni ya miaka 27 na zaidi iliyopita. Kumbukumbu zimehamishwa kutoka NBC kwenda BoT. Hata huko NBC shughuli zilikuwa zinafanywa katika matawi mbalimbali nchini tena miaka hiyo hapakuwa na kompyuta hivyo kumbukumbu zote ziliwekwa kwenye majalada. Pamoja na matatizo hayo ukaguzi wa hesabu za mwaka 2005/6 ulikamilika kwa kiwango cha kuridhisha.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Ukaguzi katika mwaka wa fedha wa 2005/2006 uliochunguzwa, katika mwaka 2005 yalifanywa malipo ya jumla ya Shilingi 133,015,186,220.74 kwa Makampuni 22 ya hapa nchini. Makampuni hayo ni: Bencon International Ltd. of Tanzania, VB & Associates Company Ltd. of Tanzania, Bina Resorts Ltd. of Tanzania, Venus Hotel Ltd. of Tanzania, Njake Hotel & Tours Ltd., Maltan Mining Company Ltd. of Tanzania, Money Planners & Consultants, Bora Hotels & Apartment Ltd., B. V. Holdings Ltd., Ndovu Soaps Ltd., Navy Cut Tobacco (T) Ltd. of Tanzania, Changanyikeni Residential Complex Ltd., Kagoda Agriculture Ltd., G&T International Ltd., Excellent Services Ltd., Mibale Farm, Liquidity Service Ltd., Clayton Marketing Ltd., M/S Rashtas (T) Ltd., Malegesi Law Chambers (Advocates), Kiloloma and Brothers na KARNEL Ltd.
Aidha, ukaguzi umebaini kwamba kati ya fedha hizo, kiasi cha Shilingi 90,359,078,804.00 zililipwa kwa makampuni kumi na tatu (13) ambayo yalitumia kumbukumbu, nyaraka na hati zilizo batili na za kugushi. Hivyo, Makampuni hayo hayakustahili kulipwa chochote. Makampuni hayo ni: Bencon International Ltd. of Tanzania, VB & Associates Company Ltd. of Tanzania, Bina Resorts Ltd. of Tanzania, Venus Hotel Ltd. of Tanzania, Njake Hotel & Tours Ltd., Maltan Mining Company Ltd. of Tanzania, Money Planners & Consultants, Bora Hotels & Apartment Ltd., B. V. Holdings Ltd., Ndovu Soaps Ltd., Navy Cut Tobacco (T) Ltd. of Tanzania, Changanyikeni Residential Complex Ltd., Kagoda Agriculture Ltd.
Aidha, ukaguzi umeendelea kubaini kuwa Makampuni tisa (9) ambayo yalilipwa jumla ya Shilingi 42,656,107,417.00 hayakuwa na nyaraka za kuonyesha stahili ya malipo na hivyo kuwafanya wakaguzi washindwe kuhakiki uhalali wa malipo hayo. Makampuni hayo ni: G&T International Ltd., Excellent Services Ltd., Mibale Farm, Liquidity Service Ltd., Clayton Marketing Ltd., M/S Rashtas (T) Ltd., Malegesi Law Chambers (Advocates), Kiloloma and Brothers na KERNEL Ltd.
Wakati huo huo Makampuni mawili, yaani, Rashtas (T) Ltd na G&T International Ltd., kumbukumbu zake za usajili katika daftari la Msajili wa Makampuni nchini hazikuweza kupatikana.
Uamuzi wa Rais
Baada ya kuipitia Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali na ya Mkaguzi wa Nje, yaani, Kampuni ya Ernst and Young, Mhe. Rais amesikitishwa na kukasirishwa na taarifa ya kuwepo vitendo vya ukiukwaji wa makusudi wa sheria, kanuni na taratibu za uuzaji wa madeni ya nje vilivyofanywa katika taasisi muhimu na nyeti kama vile Benki Kuu. Kwa hiyo, ameamua kuwa hatua za kisheria na kiutawala zichukuliwe dhidi ya makampuni na watu waliohusika na vitendo hivyo viovu.
Kwa ajili hiyo Rais ameamua yafuatayo:-
1. Ametengua uteuzi wa Dkt. Daudi A. Balali kuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania.
2. Ameagiza Bodi ya Wakurugenzi ya Benki Kuu ikutane mara moja kujadili taarifa ya ukaguzi na kuchukua hatua zipasazo za kinidhamu dhidi ya Maofisa wote wa benki, walio chini ya mamlaka yake waliohusika na kusababisha hasara hii kwa taifa.
3. Shughuli za ulipaji wa madeni katika Akaunti ya EPA zisimamishwe mara moja mpaka hapo taratibu za uhakiki na utaratibu mpya utakapotengenezwa.
4. Rais amewaagiza; Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Inspekta Jenerali wa Polisi na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, kuchunguza na kuchukua hatua zipasazo za kisheria kwa makampuni na watu waliohusika na uhalifu huu. Rais amewataka watumie ipasavyo mamlaka na madaraka waliyo nayo kwa mujibu wa sheria. Aidha, amewataka wakamilishe kazi hiyo katika kipindi cha miezi sita. Amemuagiza Mwanasheria Mkuu wa Serikali awe kiongozi wa kazi hii. Amewataka wahakikishe kuwa fedha zilizolipwa isivyo halali zinarudishwa.
5. Rais pia amemtaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kushirikiana na kuwasaidia watendaji wakuu hao wa vyombo vya dola katika kufanikisha jukumu lao hilo. “Watu wengine wenye taarifa za ziada pia wazitoe kwa Timu ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na wenzake”.
6. Kutokana na hatua ya kutengua uteuzi wa Bwana BALALI, Mhe. Rais amemteua Prof. BENNO T. NDULU (Naibu Gavana) kuwa Gavana Mpya wa Benki Kuu. Halikadhalika, amemteua Dkt. ENOS S. BUKUKU (Katibu Mkuu – Miundombinu) kuwa Naibu Gavana wa Benki Kuu (Fedha na Uchumi). Pia amemteua Ndugu Omari Chambo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu. Uteuzi huu unaanza mara moja.
(Phillemon L. Luhanjo)
KATIBU MKUU KIONGOZI
IKULU,DAR ES SALAAM09 Januari 2008
Kwanhisani ya michuzi

posted by
Augustus Fungo, University of Essex, Sainty Quays,H8/6F Lightship Way, Colchester CO2 8GY
UNITED KINGDOM
TEL.0870 7506000 EXT.1410
HOTLINE: +44794 2592894
E-mail:
augustoons@yahoo.co.uk (default)
afungo@essex.ac.uk (official)
ludefo@gmail.com (society/NGO)
augustoons@mkwawa.com (Alumni)
administrator: www.ludefo.blogspot.com
UNITED KINGDOM
TEL.0870 7506000 EXT.1410
HOTLINE: +44794 2592894
E-mail:
augustoons@yahoo.co.uk (default)
afungo@essex.ac.uk (official)
ludefo@gmail.com (society/NGO)
augustoons@mkwawa.com (Alumni)
administrator: www.ludefo.blogspot.com
No comments:
Post a Comment