BALOZI wa Uholanzi nchini, Bw. Karel van Kesteren, amewataka Watanzania kuachana na dhana kwamba watachimba utajiri kutoka ardhini kupitia sekta ya madini.Akizungumza kwenye ufunguzi wa kongamano la mwaka la wasomi na watafiti nchini lililoandaliwa na Taasisi ya Utafiti na Tathmini ya Sera za Kuondoa Umasikini (REPOA), Dar es Salaam jana, Balozi huyo alisema dhana ya uchumi bora kutokana na maliasili ni potofu na iliyopitwa na wakati."Nadhani midahalo inayoendelea juu ya sekta ya madini, imetawaliwa na dhana potofu, kwamba mtachimba utajiri kutoka ardhini, badala ya kutengeneza utajiri," alisema Balozi huyo.Alitoa mfano wa nchi za Ulaya kama Ayalandi, Uswisi na Ufini na nchi ya Morisi, Afrika, ambazo hazikuwa na maliasili ya aina yoyote, lakini kwa kupitia dhana ya kutengeneza utajiri walipata mafanikio.Majira 3.4.2008
is this true?discuss
is this true?discuss
No comments:
Post a Comment